TAARIFA ZA HALI YA HEWA
By Dayo Radio
Published on 05/05/2026 10:26
News

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini (KMD) imetangaza kuwa hali ya hewa katika kipindi cha wiki hii inatarajiwa kuwa ya mchanganyiko, ikiwa na vipindi vya mvua hasa nyakati za asubuhi na mchana.

Kwa mujibu wa utabiri huo, viwango vya joto wakati wa mchana vitakuwa kati ya nyuzi joto 29 hadi 30 za Selsiasi, huku usiku vikishuka hadi takriban nyuzi joto 24.

Aidha, upepo wa wastani kutoka kusini mashariki unatarajiwa kuvuma, sambamba na hali ya wastani ya bahari, hali itakayowezesha shughuli za baharini kuendelea kwa ujumla katika mazingira mazuri.

Wananchi wamehimizwa kuchukua tahadhari hasa wakati wa mvua, kutokana na uwezekano wa barabara kuteleza. Pia wametakiwa kuzingatia usalama wao pamoja na wa wengine wanaposafiri au kushiriki shughuli za baharini.

Mamlaka husika zimeendelea kusisitiza umuhimu wa kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Utabiri huu unahusu kipindi cha kuanzia tarehe 5 Mei hadi 11 Mei 2026.

Comments
Comment sent successfully!