MANCHESTER UNITED YATAZAMIA FAINALI YA EUROPA LEAGUE DHIDI YA ATHLETIC CLUB
United yashikilia ushindi wa mabao 3-0 kabla ya mechi ya marudiano kwenye uwanja wa nyumbani, Old Trafford
By Dayo Radio
Published on 08/05/2025 12:13
Sports

Manchester United itakabiliana na Athletic Club usiku wa leo, Alhamisi tarehe 8 Mei 2025, katika mechi ya marudiano ya nusu fainali ya UEFA Europa League katika uwanja wa Old Trafford. Mtanange huo utaanza saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

United inaingia kwenye mechi hii ikiwa kifua mbele na mabao 3 bila walio pata katika mkondo wa  kwanza mjini Bilbao. Mabao hayo yalifungwa na Casemiro pamoja na Bruno Fernandes aliyefunga mabao mawili.

Kwa upande wa Manchester United, wachezaji Diogo Dalot na Matthijs De Ligt hawatakuwepo kutokana na majeraha. Hata hivyo, Bruno Fernandes na Casemiro wanatarajiwa kurejea katika kikosi cha kwanza baada ya kupumzishwa katika mchezo uliopita.

Athletic Club inakumbwa na pigo kubwa baada ya washambuliaji wake tegemezi, ndugu Nico na Inaki Williams, kuumia. Aidha, mfungaji wao bora Oihan Sancet hajaingizwa kwenye kikosi na beki Dani Vivian yuko nje kwa sababu ya kadi nyekundu.

Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, amesisitiza umuhimu wa kikosi chake kucheza kwa umakini na kutafuta bao la mapema ili kuondoa matumaini ya wapinzani wao. Athletic Club wanahitaji muujiza kubadili matokeo hayo, lakini wana motisha kubwa kwani fainali ya Europa League mwaka huu itafanyika kwenye uwanja wao wa nyumbani, San Mamés.

Kwa hali ilivyo, Manchester United ina nafasi nzuri sana ya kufuzu fainali, huku Athletic Club wakikumbwa na majeruhi na kadi nyekundu.

Comments
Comment sent successfully!