Rais William Ruto ameipokea rasmi ripoti ya jopo la uteuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ( IEBC), katika hatua muhimu ya kuanza kwa mchakato wa kuunda upya tume hiyo.
Ripoti hiyo imewasilisha majina ya walioteuliwa kuwania nafasi ya mwenyekiti pamoja na makamishna wa IEBC. Jopo hilo la uteuzi limekuwa likifanya kazi kwa miezi kadhaa kuchambua na kuhoji wagombea mbalimbali kabla ya kuwasilisha mapendekezo yao kwa Rais.
Akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais Ruto amelisifu jopo hilo kwa, kwa mujibu wake, kazi nzuri na ya kitaalamu waliyoifanya. Ameeleza kuwa hatua inayofuata ni yeye mwenyewe kuwateua rasmi waliochaguliwa, kisha kuyawasilisha majina yao mbele ya Bunge kwa ajili ya kuidhinishwa.
Hatua hii inatarajiwa kufufua tena shughuli za IEBC, ambayo kwa muda imekuwa haifanyi kazi kikamilifu kutokana na ukosefu wa uongozi wa kudumu.