Msanii wa dancehall Vybz Kartel ameachiliwa baada ya kuhukumiwa miaka 13 gerezani kwa kosa la mauaji.
Mahakama ya Rufaa ya Jamaica iliamua kumwachilia msanii huyo akiwa na wenzake, Shawn ‘Storm’ Campbell, Andre St John, na Kahira Jones baada ya kartel kukosekana kwa ushahidi na mashahidi kwenye kesi hiyo.
Uamuzi huo pia ulitokana na hali yake mbaya kiafya na matatizo ya kifedha.
Mashabiki walikusanyika nje ya gereza la Tower Street Adult Correctional Centre huko Kingston, wakiimba "Free World Boss" kwa furaha.